- 311 viewsDuration: 3:26Miili miwili ya watu walioporomokewa na mgodi katika eneo la Ogago huko Bondo kaunti ya Siaya imeopolewa leo huku mtu wa tatu akiwa bado hajapatikana. Leo imekuwa siku ya pili ya shughuli ya uopoaji huku jamii za walioangamia ikitaka usaidizi kutoka kwa serikali. Kilio chao kinawadia wakati ambapo wachimba migodi na washikadau wakitaka sera za kulinda migodi kubuniwa baada ya watu kumi kufariki katika mgodi wa pokot magharibi.