Skip to main content
Skip to main content

Miili ya wachimbaji watatu wapatikana Bondo, Murkomen atoa wito wa usalama migodini

  • | Citizen TV
    453 views
    Duration: 2:56
    Shughuli za kutafuta wachimbaji migodi waliokwama ndani ya mgodi wa dhahabu wa Ogago katika eneo la Bondo zimekamilika baada ya miili yote mitatu kupatikana na kupelekwa katika hifadhi ya maiti ya Bondo. Haya yanajiri huku Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen aliyezuru eneo la mkasa mwingine wa mgodi huko Romus, Pokot Magharibi, akiwataka wachimbaji kuzingatia usalama wanapotekeleza shughuli zao.