Skip to main content
Skip to main content

Mikakati iliyompa Sammy Kamau ushindi wa Ol Kalou

  • | Citizen TV
    18,362 views
    Duration: 4:33
    Ushindi wa Sammy Douglas Kamau Waweru wa chama cha Democracy for Citizens Party (DCP) katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou umehusishwa na mikakati ya kisiasa iliyochanganya ujumbe wa kimantiki, kihisia na kujenga imani kwa wapigakura. Kamau alipata kura 35,440 dhidi ya kura 5,450 za mpinzani wake wa UDA, Samuel Muchina Nyaga. Inadaiwa mikakati hiyo iliratibiwa kwa wiki kadhaa, huku kampeni zikigeuza kejeli dhidi ya mgombea huyo kuwa nyenzo ya kuvutia hisia za wapigakura, kabla ya juhudi kuelekezwa katika kulinda kura hadi mwisho wa mchakato wa uchaguzi.