Mikakati yaanzishwa kukabiliana na dhulma za kijinsia eneo la Tana River

  • | Citizen TV
    55 views

    Kama njia ya kukabiliana na dhulma za kijinsia kaunti ya Tana River, serikali ikiongozwa na kamishna wa kaunti hiyo imebuni vitengo mbalimbali vya kusaidia kupunguza dhulma za aina yoyote. Baadhi ya dhulma sugu ni ukeketaji, majeraha kutokana na kupigwa, mimba za utotoni pamoja na kutopeleka watoto shuleni.