- 419 viewsDuration: 1:14Miungano inayotetea maslahi ya wanahabari nchini imeeleza wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa mashambulizi dhidi ya waandishi wa habari, matumizi ya wahuni kuvuruga shughuli za uandishi na kuzorota kwa mazingira ya kazi. Wakizungumza jijini Nairobi, viongozi wa Kenya Union of Journalists na Association of Media Women in Kenya wametaka haki kwa wanahabari walioshambuliwa wakiwa kazini, huku wakitoa wito wa kulindwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi.