Aliyekuwa mbunge wa Kilome, Harun Mwau, alifika kizimbani leo kutoa ushahidi kwenye kesi ya madai ya kuchafuliwa jina aliyowasilisha miaka 20 iliyopita dhidi ya gazeti moja la humu nchini. Mwau aliiambia mahakama kuwa makala yaliyochapishwa na gazeti hilo kati ya Disemba 2004 na mapema 2005, ilimhusisha kimakosa na ulanguzi wa dawa za kulevya, jambo alilosema liliharibu sifa yake kama mtumishi wa umma mwenye heshima na mfanyabiashara maarufu. Mwau anataka alipwe fidia ya mamilioni ya pesa kwa aibu aliyopata kutokana na taarifa hizo. Taarifa kamili ni katika kitengo cha mizani ya haki.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive