Serikali imetoa hakikisho la kujitolea kulainisha mchakato wa kutayarisha bajeti ili kuhakikisha utekelezaji murwa wa mkakati wa kitaifa wa mageuzi ya utunzi wa mwaka 2022–2032. Kulingana na waziri wa jinsia, utamaduni na huduma za watoto Hannah Wendot Cheptumo, hatua hiyo itarahisisha utangamanishaji wa watoto wanaotunzwa katika vituo vya uhisani na familia. Cheptumo aliyasema hayo wakati wa mkutano wa mashauriano na wadau jijini Nairobi ambapo alitoa wito wa juhudi za pamoja miongoni kuhakikisha watoto wanalelewa katika mazingira salama ya kifamilia.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive