Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Renson Ingonga ameishutumu Mamlaka ya kuangazia utendakazi wa polisi IPOA na idara ya upelelezi DCI kwa kukosa kuwasilisha ushahidi muhimu kuhusu kesi za madai ya polisi kukiuka sheria. Akizungumza jijini Nairobi Ingonga amesema kesi nyingi ambazo hazijakamilishwa zinawahusu maafisa wa usalama. Miongoni mwa kesi hiyo ni kisa cha polisi kudaiwa kuwapiga risasi watu wawili mtaani Kitengela na mtu mmoja Huruma na matumizi ya vitoa machozi ndani ya kanisa huko Othaya na katika mikutano ya kisiasa Kitengela na Kakamega.
“We wait for investigative agencies to submit their reports so that we can prosecute those involved,” he said, underscoring what he described as a systemic failure by oversight and investigative bodies to deliver timely findings.