Mkurungenzi wa kampuni ya SBL Innovate ahojiwa bungeni

  • | Citizen TV
    443 views

    Na kwenye uchunguzi wa sakata ya mbolea ghushi, mkurungenzi wa kampuni ya SBL Innovate Josiah Kariuki amedai kuwa bodi ya nafaka na mazao iliuza magunia laki moja ya mbolea inayodaiwa kuwa ghushi na iliyosambazwa na kampuni yake. Kariuki aliyefika mbele ya kamati ya kilimo bungeni kutoa taarifa kuhusiana na sakata hiyo, amesema kuwa NCPB ilichukua sampuli ya mbolea yake kabla ya kuanza kuiuza mwaka wa 2022. Kariuki hata hivyo alikuwa na wakati mgumu kujibu madai kuwa bidhaa aliyowauzia wakulima ni tofauti na ile iliyoidhinishwa na kebs alipopewaleseni.