- 454 viewsDuration: 11:27Huku juhudi za kudhibiti mlipuko wa Ebola unaoathiri maeneo kadhaa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda zikiendelea, Shirika la Afya Duniani WHO linasema bado kuna changamoto kubwa katika kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo. Ingawa mwitikio wa kiutendaji umeimarika katika wiki za hivi karibuni, WHO inaonya kuwa hali ya maambukizi bado inatia wasiwasi. Mwandishi wa BBC Sammy Awami amezungumza na Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Afrika, Profesa Mohamed Janabi, kuhusu hali ya mlipuko huo, changamoto zilizojitokeza na maandalizi ya nchi za jirani kukabiliana na hatari ya kusambaa kwa virusi hivyo. Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw