Skip to main content
Skip to main content

MPANGO WA KUJENGA MNARA WA KUMUENZI SHUJAA MEKATILILI WA MENZA WAZINDULIWA KILIFI

  • | KNA Video
    41 views
    Duration: 4:22
    Baraza la Kitaifa la Kutambua Mashujaa nchini limezindua mpango wa kujenga mnara katika Kaunti ya Kilifi kwa lengo la kumuenzi shujaa wa kupigania uhuru, Mekatilili wa Menza. Viongozi wa baraza hilo walizungumza na wanahabari baada ya kuzuru Shakahola, eneo lenye historia muhimu katika harakati za kupinga ukoloni. Walisema kuwa kutambua na kuenzi mashujaa wa taifa ni njia muhimu ya kuhifadhi historia ya Kenya na kuelimisha vizazi vijavyo kuhusu mchango wao katika safari ya kupata uhuru. Katika hafla hiyo, gavana wa Kilifi alipokea medali na cheti kwa niaba ya familia ya Mekatilili wa Menza kama ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika mapambano ya ukombozi.