Gavana wa Kaunti ya Garissa Nathif Jama Adam, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa uwanja mdogo wa ndege wa Garissa, akisema kuwa mradi huo uko katika hatua za mwisho kukamilika.
Gavana Nathif amesema kuwa ifikapo mwisho wa mwezi huu, uwanja huo utafunguliwa rasmi na kuanza kutumika, hatua ambayo inalenga kuboresha usafiri pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika kaunti hiyo. Wakazi wameelezea matumaini yao kuwa mradi huo utaleta fursa za ajira na kuongeza ukuaji wa uchumi katika eneo hilo.