Mswada kuhusu uvunaji mchanga wawasilishwa katika kaunti ya Kajiado

  • | Citizen TV
    163 views

    Bunge la kaunti ya Kajiado kupitia kwa kamati ya Mazingira na mali ghafi inapanga kuwasilisha mswada unaolenga kuunda sheria ya kuthibiti biashara ya uvunaji wa mchanga katika kaunti ya Kajiado. Kamati hiyo ilikutana na wadau mbali mbali waliolalamika kuhusu jinsi biashara hiyo imeachiliwa bila kuthibitiwa na hivyo kusabisha uharibifu Mkubwa wa mazingira.