Mtahiniwa mmoja wa KCSE anafanya mtihani wake katika hospitali Nakuru ambapo anatarajiwa kujifungua

  • | Citizen TV
    710 views

    Katika kaunti ya Nakuru, mtahiniwa mmoja wa KCSE anafanya mtihani wake katika hospitali ya rufaa ya Nakuru ambapo anatarajiwa kujifungua hii leo . Mkurugenzi wa elimu katika eneo la Nakuru Mashariki Job Kaikai amesema kuwa wizara ya elimu imeweka mikakati ya kumfikishia mwanafunzi huyo mtihani kwa wakati unaofaa. Watahiniwa laki moja elfu saba mia tano ishirini na tisa katika kaunti ya Nakuru wanafanya mtihani wa Kiingereza na Kemia hii leo.