Mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne (KCSE) wa mwaka huu umeanza rasmi, huku wanafunzi wakifanya mitihani ya mahojiano na vitendo. Mitihani ya vitendo inatarajiwa kukamilika tarehe 31 mwezi Oktoba, kabla ya kuanza kwa mitihani ya maandishi tarehe 4 mwezi ujao. Jumla ya watahiniwa 996,078 wanafanya mtihani huo katika vituo 10,765 kote nchini. Mwanahabari wetu Joseph Wakhungu anaangazia ratiba ya mtihani huo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive