Mtoto wa miaka-3 anajisiwa na kuuawa Murang'a

  • | KBC Video
    113 views

    Matokeo ya uchunguzi wa maiti ya Eliza Wamaitha, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, aliyepatikana akiwa amefariki katika kinamasi Jumatatu iliyopita, yalifichua kuwa alibakwa huku sehemu zake za siri zikiwa zimejeruhiwa vibaya na kichwa chake kugongwa na kifaa butu, hali iliyosababisha kifo cha ghafla. Kulingana na mtaalamu wa uchunguzi wa maiti wa serikali Dkt. Waithira Mbau, hakukuwepo na dalili za kuashiria kuwa alinyongwa shingoni wala kuzama majini. Uchunguzi huo ulibaini kwamba msichana huyo mchanga tayari alikuwa amefariki alipotupwa kwenye kidimbwi hicho cha maji.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive