- 39,412 viewsDuration: 1:59Kwa vijana wengi, kilimo si chaguo lao la kwanza la kujenga maisha. Lakini kwa Valentina Moi, mwenye miaka 24, kilimo kimekuwa biashara, ajira na fursa ya kuwawezesha wengine. Licha ya changamoto za kuwa mwanamke kijana katika sekta hiyo, Valentina tayari amewafundisha zaidi ya vijana elfu mbili kuhusu kilimo biashara. Lakini kwa nini alichagua kilimo, na ni changamoto zipi amekutana nazo njiani? Mwandishi wa BBC @scolarkisanga amezungumza na bi Valentina katika makala ya Waridi wa BBC na kutuandalia taarifa hii. š„: @frankmavura - - #bbcswahili #kilimo #waridi #waridiwabbc Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw