Muungano wa Azimio umepuuzilia mbali tetesi za ugovi baina ya viongozi wa vyama tanzu vya muungano

  • | K24 Video
    56 views

    Muungano wa Azimio unasema sasa uko imara na umepuuzilia mbali tetesi za ugovi baina ya viongozi wa vyama tanzu vya muungano huo. Hii ni licha ya vuta ni nikuvute iliyoshuhidiwa wiki jana kuhusu ugavi wa nafasi za tume ya huduma kwa bunge (PSC). Wabunge wa vyama tanzu vya muungano huo wamesema kuwa vinara wa muungano huo akiwemo Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Uhuru Kenyatta wamefanya mazungumzo na kukubailiana kuhusu mustakabali wa muungano.