Muungano wa Maafisa Kliniki nchini KUCO umekosoa vikali serikali ya kaunti ya Marsabit kutokana na mgomo unaoendelea wa maafisa wa kliniki ambao wanasema umelemaza huduma za afya katika kaunti hiyo. Mwenyekiti wa muungano huo Peterson Wachira ameibua wasiwasi kuhusu ongezeko la vifo vya watoto wachanga katika kaunti hiyo, akisema kuwa hali hiyo inachochewa na mgomo huo uliodumu kwa siku 151 sasa.
Maafisa wa kliniki walianza mgomo huo miezi sita iliyopita kushinikiza utekelezaji wa makubaliano ya awali ya kurejea kazini, huku wakiongeza kuwa serikali ya kaunti imedinda kurejea kwa mazungumzo. Muungano huo pia unaishutumu kaunti hiyo kwa kusitisha mishahara ya wanachama wake licha ya mgomo kuwa halali . Sasa maafisa hao wanatoa wito kwa Seneti kuingilia kati na kumaliza mvutano huo, ambao wanasema umeathiri kwa kiasi kikubwa utoaji wa huduma za afya katika kaunti hiyo...