Skip to main content
Skip to main content

Mvutano wa Kitui na Garissa waathiri usafiri na biashara

  • | Citizen TV
    7,963 views
    Duration: 3:31
    Hali ya utulivu bado haijarejea katika mpaka wa kaunti za Kitui na Garissa huku mzozo kati ya jamii mbili jirani ukiendelea kutokota na kuathiri shughuli za usafiri na biashara. Barabara ya Mwingi–Garissa imeendelea kuwa tete kwa siku ya tatu mfululizo, hali ambayo imesababisha kufungwa kwa barabara hiyo muhimu. Abiria kadhaa bado wamekwama katika vituo vya mabasi jijini Nairobi na Garissa baada ya wahudumu wa usafiri kusitisha huduma kwa hofu ya usalama.