Skip to main content
Skip to main content

Mwanafunzi aliyeangamia kwenye moto wa Utumishi Academy azikwa Kwale

  • | Citizen TV
    3,481 views
    Zuhra Rama Higa, mmoja wa wanafunzi 16 walioangamia katika mkasa wa moto katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Utumishi Academy huko Gilgil, amezikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Mkwakwani, Kaunti ya Kwale. Familia yake ndiyo ya kwanza kukabidhiwa mwili wa mpendwa wao kwa ajili ya mazishi, kwa kuzingatia taratibu za dini ya Kiislamu. Wanafamilia hao wanaitaka haki kutendeka kwa waliofariki kwa kuwachukulia hatua kali wote watakaopatikana na hatia ya kuhusika na mkasa huo. Aidha, familia hiyo imesema haijapata msaada wa moja kwa moja kutoka kwa serikali tangu kutokea kwa mkasa huo.