Mwanafunzi wa gredi ya pili afariki maji Nakuru

  • | Citizen TV
    477 views

    Mwanafunzi wa gredi ya pili katika shule ya msingi ya Lenana jijini Nakuru amefariki baada ya kusombwa na maji alipokuwa anatoka shuleni. Ripoti za maafisa wa usalama zinaarifu kuwa glen karanja alikuwa anavuka mtaro kando ya barabara alipoteleza.mwili wake ulipatikana mita chache kutoka eneo la tukio. Mwili wa mtoto huyo wa miaka minane unahifadhiwa kwenye makafani ya hospitali ya rufaa ya Nakuru.