Mwanafunzi wa shule ya Chavakali afariki kwenye ajali

  • | Citizen TV
    7,713 views

    Familia ya mwanafunzi wa shule ya upili ya chavakali aliyefariki kwenye ajali ya barabarani imeilaumu shule hiyo kwa kuwaachilia wanafunzi kusafiri wakati wa usiku. Familia hiyo inasema wazazi wa wanafunzi hawakukubaliana na shule kuwaruhusu watoto hao kuabiri basi usiku ila shule iliendelea na mipango hiyo. Familia ya Joseph Maduli mwenye umri wa miaka 17 inasema ilipokea habari za kifo cha mwanao kupitia mitandao ya kijamii. Na inalaumu usimamizi wa shule kwa kutotoa maelezo kuhusu kufariki kwa mwanao.