Mwanahabari Zubeidah Koome ashinda urais wa chama cha wahariri nchini

  • | KBC Video
    1,793 views

    Mwanahabari Zubeidah Kananu wa runinga ya KTN amechaguliwa tena kuwa rais wa chama cha wahariri humu nchini. Kananu alipata kura 72 akimpiku mpinzani wake Yvonne Okwara, wa runinga ya Citizen ambaye alipata kura 58 katika uchaguzi ulioandaliwa leo kupitia kwa njia ya mtandao. Naibu mhariri mkuu wa runinga ya KBC Millicent Awuor, alichaguliwa bila kupingwa kuwa mwanachama wa kitengo cha runinga katika baraza la chama hicho, huku Agnes Mwangangi ambaye ni mhariri na msomaji wa habari wa radio akichaguliwa kuwa mwanachama katika kitengo cha redio kwenye baraza la chama hicho. Asilimia 96.3 ya wapiga kura walishiriki katika uchaguzi huo

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive