Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi azuiliwa Tanzania

  • | Citizen TV
    3,574 views

    Mwanaharakati wa Kenya Boniface Mwangi angali amezuiliwa na maafisa wa polisi wa Tanzania. Inaarifiwa kuwa Mwangi anatarajiwa kurejeshwa nchini Kenya, kwenye hatma iliyowaksibu wanaharakati na mawakili sita wa Kenya walioingia nchini humo kusimama na kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Haya yanajiri huku wanaharakati nchini Kenya wakiandamana leo, wakikashifu hatua ya rais wa Tanzania Samia Suluhu kuwanyima wakenya kibali kuingia nchini humo.