- 76 viewsKwa zaidi ya miaka ishirini, amekuwa mwenyeji katika hospital ya Coast General, shughuli zake zikijikita katika jiko la hospitali hiyo. Japo hakupangia kufanya kazi ya upishi, ari ya kujikimu kimaisha ilimsukuma katika ulingo ambao hakutegemea utakuwa taaluma yake. Namzungumzia Wahida Sudi ambaye bidii yake imempandisha hadi kuwa mpishi mkuu katika hospitali ya Makadara, kazi ambayo anasema anaiheshimu na kuienzi kila uchao.