Skip to main content
Skip to main content

Mwanamke Bomba | Rosebella Ojiambo: Kutoka ndoto ya elimu hadi kujenga mtandao wa shule

  • | Citizen TV
    1,147 views
    Duration: 5:48
    Huku kina mama wengi wakitambulika kwa mchango wao katika kuinua na kujenga jamii, Rosebella Ojiambo aliamua kuwekeza katika elimu bora kwa watoto wake, akiamini kuwa mama ndiye mwalimu wa kwanza katika maisha ya mtoto. Azma yake ya kuhakikisha watoto wanapata elimu bora ilimsukuma kuanzisha shule ya Good Testimony, ambayo sasa imekua na kuwa mtandao wa zaidi ya shule tano jijini Nairobi na maeneo ya viungani. Katika makala yetu ya Mwanamke Bomba wiki hii, Rosebella anasimulia safari yake ya kuanzisha na kukuza biashara ya shule za Good Testimony, ambazo si tu zimechangia utoaji wa elimu bali pia zimekuwa chanzo cha ajira na riziki kwa wengi.