2,326 views
Duration: 2:38
Taharuki ilitanda katika Mahakama ya Bungoma baada ya mzee mmoja aliyekuwa akisubiri kusikilizwa kwa kesi ya mzozo wa ardhi kufariki nje ya mahakama hiyo. Idara ya Mahakama imesema kuwa marehemu aliwasili mahakamani akionekana kuwa katika hali mbaya ya kiafya, na kesi yake ikapewa kipaumbele kusikilizwa. Hata hivyo, aliamua kupumzika nje ya mahakama akimsubiri wakili wake lakini baadaye akapatikana bila fahamu. Polisi walithibitisha kifo chake muda mfupi baadaye. Kaka yake marehemu amesema kuwa alikuwa anaugua maradhi ya moyo.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive