Mwanaume ajaribu kujiua baada ya kumkata mkewe mkono

  • | Citizen TV
    422 views

    Mwanaume mmoja amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Baringo baada ya jaribio la kujiua kutibuka. Laban Kipchumba, mwenye umri wa makamo, alijaribu kujitoa uhai baada ya kumkata mkewe mkono kwa panga. Anadaiwa kuwa waili hao walikuwa wamezozana kuhusu mwanao kukosa kurejea nyumbani baada ya mamake kumpeleka kwa nyanyake. Mwathiriwa, Veronica Jepkoech, ambaye ni mama wa watoto wawili, pia anapokea matibabu katika hospitali hiyo.