Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Nairobi Prof. Amukowa Anangwe na wengine watatu wachunguzwa

  • | Citizen TV
    1,531 views

    Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Nairobi, Profesa Amukowa Anangwe pamoja na maafisa wengine watatu waandamizi walikamatwa Ijumaa na maafisa wa Kupambana na Ufisadi (EACC) na kushtakiwa kwa matumizi mabaya ya mamlaka. Profesa Anangwe na wanachama wengine wa baraza la chuo hicho wanatuhumiwa kutumia mamlaka vibaya kuhusiana na uteuzi usio halali wa Brian Ouma kuwa Kaimu Afisa Mkuu wa operesheni katika Chuo hicho.. wanne hao wameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki tano kila mmoja huku uchunguzi ukiendelea.