Mwili umepatikana bila kichwa mtoni Tana

  • | Citizen TV
    2,087 views

    Polisi katika mji wa Madogo kaunti ya Tana River wanachunguza kisa cha kushangaza ambapo maiti isiyokuwa na kichwa ilipatikana ikielea katika mto Tana. Mwili huo wa mwanaume uliopatikana na wafugaji waliokuwa wakilisha mifugo wao kando kando ya mto huo pia ulikuwa na majeraha ya panga kwenye mkono wa kushoto. Wenyeji sasa wanalalamikia kuongezeka kwa visa vya maiti kutupwa katika mto huo. Mwaka jana maiti 19 ziliopolewa kwenye mto huo.