Mwili wa mtoto wazuiliwa kwa zaidi ya mwaka mmoja hospitalini

  • | Citizen TV
    902 views

    Familia moja kutoka kijiji cha Nyamarambe kaunti ya Kisii inataabika baada ya kushindwa kuuzika mwili wa mtoto wao uliozuiliwa katika makafani moja mjini Eldoret kwa muda wa zaidi ya mwaka moja unusu sasa. Familia hiyo pamoja na kijiji kizima wamechangisha shilingi elfu 30 pekee baada ya bili kufikia shilingi milioni 3.4. Na kama anavyoripoti mwanahabari wetu Chrispine Otieno mila na tamaduni za jamii ya Abagusii zimekuwa kikwazo katika shughuli hiyo.