Skip to main content
Skip to main content

Mwimbaji wa Iran Parastoo Ahmadi amehukumiwa viboko 74

  • | BBC Swahili
    11,302 views
    Duration: 1:16
    Mwimbaji wa Iran Parastoo Ahmadi amehukumiwa viboko 74 kwa kutumbuiza bila kuvaa hijabu katika tamasha mwaka 2024. Nchini Iran, wanawake wanakabiliwa na vikwazo vikali linapokuja suala la kuimba na kutumbuiza hadharani. Parastoo aliandaa tamasha la “kufikirika” (imaginary concert) kama njia ya kupinga vikwazo hivyo, kisha akashiriki video ya onyesho lake mtandaoni. Watu wengine wanane, wakiwemo wanamuziki, pia wamepewa adhabu hiyo ya viboko 74. Mwandishi wa BBC @frankmavura na taarifa zaidi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw