- 91 viewsDuration: 1:50Serikali ya kaunti ya Mombasa pamoja na wasanii katika ukumbi wa sanaa wa little theatre wametaka mwafaka kati yao na shirika la reli kuhusu kipande cha ardhi wanachopania kujenga taasisi ya mafunzo. Kulingana na mwenyekiti wa ukumbi huo Daudi Anguka wasanii hawatakubali kufurushwa na kuwa makubaliano ni sharti yazingatie kuwepo kwa wasanii baada ya mradi huo. Gavana wa mombasa kwa upande wake ametaka serikali ya kaunti kushirikishwa ili kuhakikisha kuwa usawa umeafikiwa.