Mzozo wa ardhi katika eneo la Gatia, katika eneo la Ruai, kaunti ya Nairobi,unatishia ujenzi wa shule mpya ya msingi ya umma, inayokusudiwa kupunguza msongamano na kupunguza umbali ambao watoto hutembea ili kupata elimu. Wakazi wanadai kuwa, ardhi hiyo ilikuwa imesalimishwa na kampuni ya mashamba ya Embakasi, ili kupisha ujenzi wa shule ya msingi ya Gatia, inagawanywa na kupewa wajenzi wa kibinafasi. Hatahivyo madai hayo hayajathibitishwa. Mzozo huo umeathiri utekelezwaji wa ufadhili wa shilingi milioni 15 wa mradi huo wa shule kupitia hazina ya serikali ya kitaifa ya maendeleo ya eneo bunge la Kasarani.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive