Nani mnufaika wa uchaguzi usio na upinzani wenye nguvu Tanzania?

  • | BBC Swahili
    1,685 views
    Kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani zimeanza rasmi nchini Tanzania. Chama tawala, Chama Cha Mapinduzi CCM, kimemsimamisha Rais Samia Suluhu Hassan akiwania muhula mwingine, na mgombea mwenza wake Dr. Emmanuel Nchimbi. Hata hivyo, Chama kikuu cha upinzani Chadema kimesusia uchaguzi huo, huku kiongozi wake Tundu Lissu akiwa mahabusu kwa tuhuma za uhaini zinazotokana na madai ya kupanga uasi. Wakati huo huo, chama kingine cha upinzani, ACT Wazalendo, kimefungua kesi katika Mahakama Kuu kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi kumuengua mgombea wake wa Urais, Luhaga Mpina. #bbcswahili #tanzania uchaguzi2025 Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw