Natembeya ataka IPOA kupewa mamlaka zaidi

  • | Citizen TV
    1,013 views

    Gavana wa Kaunti ya Trans Nzoia, George Natembeya, ameomba serikali kuu kuipatia nguvu zaidi mamlaka ya utendakazi wa polisi -IPOA- ili iweze kuwakamata na kuwafungulia mashtaka maafisa wa usalama wanaotumia nguvu kupita kiasi wanapotekeleza majukumu yao. Akitaja visa vya mauaji ya watu watano kaunti ya Narok mapema wiki hii, pamoja na maafa wakati wa maandamano ya kizazi cha GEN Z, Natembeya amesema kuwa maafisa wengi hujihusisha na ukatili dhidi ya raia lakini hawachukuliwi hatua za kisheria licha ya uchunguzi kufanywa na IPOA. Amedokeza kuwa hali hii imepelekea wananchi kukosa imani na vyombo vya usalama, akisisitiza haja ya kuwajibisha wote wanaokiuka sheria.