- 16,517 viewsDuration: 20:53Mwandishi wa BBC Swahili Sammy Awami alipata nafasi ya kipekee kutembelea gereza linalowashikilia wafungwa wa kivita huko Ukraine. Serikali ya Ukraine imeiambia BBC kuwa kwa sasa kuna karibu wapiganaji 3,000 kutoka Afrika wanaohudumu katika jeshi la Urusi, wengi wao wakidaiwa kudanganywa au kulazimishwa kujiunga na vita kupitia mawakala haramu wa uajiri waliowaahidi kazi nzuri na mishahara mikubwa nchini Urusi. Baadhi ya wanaume hao wamefariki vitani, wengi hawajulikani walipo, huku wengine wakiwa wameshikiliwa na Ukrainę kama wafungwa wa kivita. #bbcswahili #ukrainerussia #kenya Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw