- 8,928 viewsDuration: 59sNdugu wawili wamefariki baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzidiwa na mawimbi makali ya bahari na kuzama katika Bahari Hindi, Kaunti ya Mombasa. Wawili hao, kaka na dada, walikuwa miongoni mwa familia ya watu watano waliotembelea Mombasa kutoka Magharibi mwa Kenya kwa ajili ya kujivinjari. Boti hiyo inadaiwa kukodishwa na familia hiyo kutoka hoteli moja eneo la Nyali na ilikuwa ikielekea Fort Jesus kabla ya ajali hiyo. Miili ya marehemu inahifadhiwa katika makafani ya Hospitali ya Coast General.