Ni nani ananufaika zaidi klabu za mpira kutumika kisiasa?

  • | BBC Swahili
    773 views
    Kwa miaka mingi, klabu kongwe za soka Tanzania Yanga na Simba zimekuwa zaidi ya timu za mpira; zimekuwa jukwaa la siasa, kusaka umaarufu na daraja la mafanikio ya kisiasa kwa baadhi ya viongozi. Hata hivyo, kuna hatari ya klabu kutumika kisiasa bila kupata faida ya moja kwa moja kama vile wanasiasa kutumia jina la klabu kujinufaisha kisiasa bila kuwekeza au kusaidia maendeleo ya klabu hizo. Swali la msingi linaibuka: Ni nani ananufaika zaidi klabu au siasa? Ungana na Mwandishi wa BBC @eagansalla_gifted_sounds akilichambua hili kinagaubaga. 🎥: Frank Mavura #bbcswahili #tanzania #siasa Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw