'Ninaulizwa kila mara juu ya kufikia wadhifa wa Jenerali, sikuwa nimefikiria'

  • | VOA Swahili
    350 views
    [[Ni mtoto wa wazazi kutoka Zimbabwe na Nigeria na hivi leo anahudumu kama mtunukiwa wa cheo cha Naibu Jenerali msimamizi katika kituo cha Mafunzo ya Ukadeti huko Fort Knox, Kentucky. Mwandishi wa VOA Grace Oyenubi akizungumza na Brigedia Jenerali Amanda Azubuike, kiongozi wa kijeshi.]] ... "Jina langu ni Amanda Azubuike. Mimi ni naibu kamanda jenerali wa Mafunzo ya Ukadeti. Wakati wa kipindi cha joto, nina hudumu katika kituo cha mafunzo ya Ukadeti. Vizuri, kwanza kabisa, sikuwahi kufikiria nitakuwa hapa. Ninaulizwa kila mara juu ya kufikia wadhifa wa Jenerali. Sikuwa nimefikiria. Kwa hiyo siku nilipopokea nyota yangu. Nilihisi nimepewa heshima kubwa. Natambua umuhimu wa wakati huu, natambua majukumu, matarajio na pia tathmini inayokuja na cheo hiki. Na pia natambua mamlaka ya uwakilishi na umuhimu wa mchanganyiko ulioko katika timu hizi. Ilikuwa ni furaha yenye uchungu kwangu kwa sababu wazazi wangu wote ni marehemu." Kwa hiyo mara moja unafikiria kuhusu watu wote waliokusaidia kufika hapo, na kusema kwa jumla katika lililo juu ya orodha hiyo ni familia. #VOASwahili #naibujenerali #mmarekani #jeshi #chuochamafunzo #ukadeti #voa #amandaazubuike Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.