Skip to main content
Skip to main content

Nyongeza ya malipo ya majani chai Kandara Muranga

  • | Citizen TV
    24 views
    Wakulima wa majani chai katika Eneo bunge la Kandara, Kaunti ya Murang’a, wamepokea kwa furaha tangazo la kuongezwa kwa malipo ya kila mwezi ya majani chai na Shirika la majani Chai Nchini, KTDA kutoka shilingi ishirini na tano hadi thelathini kwa kilo. Hatua hii inalenga kuboresha mapato ya wakulima kupitia mageuzi yanayoendelea katika sekta ya majani chai. Ongezeko hili ni sehemu ya mageuzi yanayoendelea katika sekta ya majani chai, yanayolenga kuongeza mapato ya wakulima, kudhibiti ushawishi wa mawakala na kuhakikisha wakulima wananufaika zaidi kupitia uongezaji thamani wa zao hilo.