- 2,558 viewsDuration: 3:03Zaidi ya nyumba 30 zimechomwa Transmara kaunti ya Narok huku idadi ya watu wasiojulikana wakiachwa na majeraha kufuatia mapigano mapya yaliyozuka katika eneo la Angata Barrikoi. Mapigano haya ya punde kati ya jamii mbili hasimu zinazoishi eneo hilo yakisababishwa na mzozo wa shamba. Kwa sasa, mamia ya watu wamelazimika kuhamia maeneo yaliyo salama ikiwemo kutafuta hifadhi kwenye shule za eneo hilo.