- 6,305 viewsDuration: 2:53Kinara wa ODM Oburu Oginga sasa anawataka wanaokinzana na msimamo wa chama kuondoka mara moja. Akizungumza katika kaunti ya Siaya, Oginga alisema kuwa chama cha chungwa lazima kiwe katika serikali ijayo na kuwa mazungumzo yataanza hivi karibuni. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, viongozi wengine pia walizomea mrengo unaoongozwa na seneta wa Nairobi Edwin Sifuna wakisema unatoa mwelekeo potovu kwa wanachama wa ODM.