- 11,487 viewsDuration: 3:02Mvutano kati ya mirengo miwili ya chama cha ODM unaendelea kutokota huku sasa Gavana wa Siaya James Orengo Sasa akijitangaza kuwa ndiye kinara asili wa chama cha chungwa. Orengo anasema kuwa mrengo wa linda mwananchi utaendelea na mikutano yake licha ya vitisho kutoka kwa baadhi ya viongozi wa ODM. Akizungumza jijini Kisumu, Orengo alipuuzilia mbali vitisho kuwa mikutano inayopangiwa kufanyika Vihiga Jumamosi na Kisumu Jumapili itakumbwa na vurugu. Na kama anavyoarifu Laura Otieno, mbunge wa Alego Usonga Samuel Atandi ametishia kuandamana na wakazi kuwakabili viongozi wa Linda Mwananchi iwapo watamkosea heshima Dkt Oburu Oginga.