Skip to main content
Skip to main content

Poiisi watumia vitoa machozi kuwatawanya wakazi wanao pinga ujenzi wa shule

  • | Citizen TV
    2,567 views
    Duration: 2:15
    Polisi katika eneo la Mukutani, Kaunti ya Baringo Kusini, walilazimika kufyatua risasi hewani Jumatatu baada ya wananchi wenye hasira kuzuia usafirishaji wa vifaa vya ujenzi wa Shule ya Msingi ya Loramoru. Vifaa hivyo, ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa katika Kituo cha Polisi cha Mukutani kwa zaidi ya mwezi mmoja kufuatia mvutano wa muda mrefu, vilikuwa vikisafirishwa kwenda Loramoru wakati sehemu ya jamii iliyopinga ujenzi huo ilipoanza kuwarushia mawe msafara huo. Shule ya Msingi ya Loramoru ilikuwa imefungwa kwa takriban miaka 13 kutokana na ukosefu wa usalama katika eneo hilo, na ilifunguliwa tena miaka miwili iliyopita baada ya hali ya usalama kuimarika.