- 18,197 viewsDuration: 30sTazama operesheni ya hatari ambapo afisa wa polisi Afrika Kusini alishushwa na helikopta hadi chini kwenye Mto Komati ili kumfunga na kupanda naye juu mamba aliyekufa ambaye inaaminika alikuwa na mabaki ya mfanyabiashara aliyepotea. Mamlaka zilisema kuwa ruhusa ilitolewa kumuua mnyama huyo kabla ya kufungwa na kusafirishwa kwa ndege hadi eneo jingine. Video inamuonyesha Kapteni John Potgieter akiwa amenining’inia hewani kwa mita kadhaa, akishikilia kamba baada ya kumfunga mnyama huyo kutoka Mto Komati. Sehemu za mwili zilizopatikana ndani ya tumbo lake zinafanyiwa uchunguzi wa DNA ili kuthibitisha utambulisho wa mwathiriwa. Mfanyabiashara huyo alikuwa amepotea kwa zaidi ya wiki moja. #bbcswahili #DNA #afrikakusini Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw