- 1,256 viewsPolisi katika Kaunti ya Kisii wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji ya mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Kenyatta. Kwa mujibu wa familia, kijana huyo kwa jina Elijah Gichogo Nyambega alitekwa nyara na watu wasiojulikana kabla ya mwili wake kupatikana siku tatu baadaye kando ya barabara. Familia na wakazi sasa wanaitaka serikali kuongeza juhudi za uchunguzi ili kuwabaini waliohusika na kuhakikisha haki inapatikana.