Picha za CCTV ambazo runinga ya Citizen imezipata zinaonyesha jinsi wanafunzi wanaodaiwa kuhusika na kuteketeza bweni katika Shule ya Wasichana ya Utumishi, Gilgil, walivyotekeleza kitendo hicho usiku wa Jumatano.
Kulingana na wapelelezi wa DCI wanaoongozwa na Martin Nyuguto, washukiwa wanane wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho, akiwemo mshukiwa mkuu anayehusishwa na upangaji wa tukio hilo.
Mwanahabari wetu Franklin Wallah anachambua yaliyomo kwenye kanda hiyo ya CCTV na hatua ambazo zimechukuliwa na maafisa wa uchunguzi kufuatia mkasa huo.