Cecilia Wanjiku ni mmoja wa wanafunzi ambao ujasiri na ushujaa wao hautasahaulika na utasalia kwenye kumbukumbu za mkasa wa moto katika shule ya wasichana ya Utumishi. Japo Cecilia ni miongoni mwa wasichana 16 waliofariki kwenye mkasa huo, alijitolea kuwaokoa wanafunzi wenzake kutoka kwenye mkasa huo ila mwenyewe hakuweza kuondoka aliwa hai. Familia yake imetambua mwili wake kwenye makafani ya hospitali ya Naivasha. Cecilia, aliyekuwa na umri wa miaka 17 ametajwa kuwa shujaa aliyehatarisha Maisha yake kuwaokoa wenzake